Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetabiri mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha siku tatu mfululizo kuanzia Novemba 8, hadi Novemba 10, 2020.
Maeneo yanayotakiwa kuwa na tahadhari kubwa ni Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.
Athari zinazoweza kujitokeza ni mafuriko kwenye makazi ya watu, baadhi ya barabara kufungwa na shughuli za kiuchumi kusimama.