Trump Akataa Ushindi wa Biden



Baada ya kusubiri kwa muda matokeo ya uchaguzi ambayo yametangazwa jana,  Donald Trump amekataa kushindwa na Joe Biden katika uchaguzi Mkuu wa Marekani na amelalamikia mapungufu mengi yaliojitokeza.

Trump atafikisha malalamiko yake Mahakamani, lakini atapata changamoto ya kuthibitisha madai yake kwakuwa wenzake ndani ya chama wameonekana kukubali.

Katika kutokubali matokeo, Trump amekuwa akituma jumbe kwenye mitandao ikiwemo Twitter, ambapo ‘tweets’ zake zimekuwa zikifutwa au kuongezewa kiunga kingine.

Biden ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Barack Obama anasubiri kuthibitishwa rasmi kwa matokeo yaliyotolewa na vyombo vya Habari.


Ushindi wa Biden unamfanya Donald Trump, kuwa Rais wa tatu katika miongo minne iliyopita kushindwa kuchaguliwa tena muhula wa pili.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad