Donald Trump amekubali kuanza kwa mchakato rasmi wa kumkabidhi madaraka Rais mteule Joe Biden.
Rais amelitaka shirika linaloshughulikia mabadilishano hayo "lifanye kile kinachostahili kufanywa", hata wakati anaahidi kuendelea kupinga matokeo.
Ofisi ya utawala wa huduma za serikali imesema inamtambua Bwana Biden kama "mshindi".
Hilo linawadia wakati Bwana Biden meidhinishwa rasmi kama mshindi wa jimbo la Michigan na kuwa pigo kubwa kwa Trump.
Timu ya Bwana Biden imefurahishwa na kuanza kwa mchakato huo wakati rais mteule anajiandaa katika sherehe za kuapishwa Januari 20.
"Uamuzi wa leo ni hatua iliyohitajika kuanza kukabiliana na changamoto zinazokumba taifa letu ikiwemo kudhibiti ugonjwa wa virusi vya corona na kuboresha uchumi tena," taarifa iliyotolewa imesema.
"Uamuzi huo ni hatua ya kiutawala ya kuanza rasmi kwa mchakato wa mabadilishano ya madaraka na mashirika husika."
Mapema Jumatatu, Bwana Biden alizindua timu itakayoangazia sera ya fedha na usalama wa taifa iliyojumuisha watu wa zamani wa miaka hiyo katika utawala wa Obama.
Biden atamchagua Anthony Blinken kuwa waziri wa mambo ya nje na John Kerry kama mjumbe wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, huku Janet Yellen ikidokezwa kwamba ndiye atakayekuwa mwanamke wa kwanza kuwa waziri wa fedha.