Twitter imezindua huduma mpya ulimwenguni inayoitwa 'fleets': tweets ambazo hupotea baada ya saa 24, sawa na machapisho kwenye Snapchat na Instagram.
Twitter hapo awali ilitangaza mpango wake wa tweets hizi za muda, zilizopewa jina la "fleet", na kufanyia majaribio huduma hiyo huko Brazil, Italia, India, na Korea Kusini.
"Baadhi yenu mnatuambia kuwa kutumia twitter ni wasiwasi kwa sababu inahisiwa kuwa ni kujianika zaidi, ni ya kudumu, na vile kuna shinikizo kubwa la kusisitiza ujumbe uliopendwa kwa kuuchapisha tena (retweet) na kupenda (like)," Mkurugenzi wa ubunifu wa Twitter, Joshua Harris, na meneja bidhaa, Sam Haveson, aliandika katika chapisho la blogu.
"Kwakuwa ujumbe unatoweka baada ya siku moja, hatua hii itawasaidia watu kujiamini kuweka taarifa na mawazo yao pia hisia zao."
Baadhi ya watumiaji wa Twitter waliokuwa wakifanyia majaribio huduma hii wamesema mtandao huo ulikuwa unasababisha wasiwasi wa uwezekano wa kudhalilishwa mtandaoni, kwa kuruhusu ujumbe wa moja kwa moja usiohitajika. Pia ujumbe kuwafikia watu uliowafungia kupata taarifa.
Twitter imesema ilikua ikipokea mrejesho na kufanyia kazi masuala yanayogusa usalama wa watumiaji wa mtandao huo.
"Fleets" zinaweza kujumuisha maandishi, picha na video. Vitapatikana kwa watumiaji kwenye mfululizo wa matukio ya picha, maandishi na video za matukio ( timelines) kwenye Twitter na maelezo kuhusu mtumaji ( profile)
Twitter na makampuni mengine ya mitandao ya kijamii iko kwenye shinikizo kubwa kudhibiti matumizi mabaya na upotoshaji wa taarifa unaosambaa. Msemaji wa Twitter Liz Kelley amesema "fleets" zitakuwa na masharti yale yale kama ilivyo kwa machapisho ya kuwekwa twitter.
Kelley amesema kuwa tahadhari- ambazo imeanza kuziweka kwenye maudhui kama vile taarifa za uongo na taarifa potofu kwa mfano Covid-19 zinaweza pia kuwekwa kwenye "fleet"
Twitter imethibitisha kuwa ilikuwa ikifanyia kazi sauti zinazoingia moja kwa moja za , ziitwazo Spaces, ambayo itafanyiwa majaribio hivi karibuni. Spaces itaruhusu watumiaji kufanya mazungumzo wakiwa kwenye kikundi. inafanana na Clubhouse, jukwaa linalotumia mazungumzo ya sauti kwenye kikundi.
"Awali mwaka huu Twitter ilianzisha mfumo wa watumiaji kuchapisha sauti kwenye mtandao huo.