UAE yasitisha utoaji viza kwa Kenya na mataifa mengine 12 ya Kiislamu





Kulingana na nyaraka iliotolewa, nchi nyingi zilizoathirika ni za Kiislamu yaani Iran, Syria, Afghanistan na Pakistan.
Chanzo cha ndani kilichozingumza na shirika la habari la Reuters kimesema chanzo cha kusitishwa kwa utoaji visa ni sababu za kiusalama lakini hakuna taarifa zozote za kina zilizotolewa.

Nyaraka hiyo iliotumwa kwa makampuni yanayoendesha shughuli za visa iliyoonesha kwamba inaanza kutekelezwa Novemba 18.

Aidha, nyaraka hiyo pia ilionesha marufuku ya kutolewa kwa visa mpya za ajira pamoja na za raia wa kigeni nje ya UAE, wanaotaka kutembelea nchi hiyo wa nchi 13 pamoja na Somalia, Libya na Yemen hadi siku isiyojulikana.

Serikali ya Kenya bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na hatua hiyo sawa na mamlaka husika ya UAE ambayo baada ya kuzungumza na Shirika la Habari la Reuters haikusema lolote.

Hatua hiyo inawadia wiki moja baada ya Ubalozi wa Ufaransa nchini UAE kusihi raia wake kuchukua tahadhari baada ya kutokea kwa shambulizi la bomu dhidi ya wanadiplomasia nchini Saudi Arabia huku wanamgambo wa Islamic State wakadai kuhusika.

Kashfa ya dhahabu Kenya

Mwaka 2019 uhusiano kati ya Kenya na UAE uliathirika kufuatia kashfa iliozunguka biashara ya Dhahabu iliokuwa ikielekea katika taiafa hilo la Kiarabu

Mtawala wa Dubai Sheikh Mohammed Al-Makhtoum, alituma barua ya pingamizi kwa Kenya akitaka kuachiliwa kwa mzigo wa dhahabu uliokuwa ukizuiliwa na idara ya forodha mjini Nairobi.

Kesi hiyo ndio ya hivi karibuni inayowahusisha washirika wa Sheikh al-Makhtoum ambao wamehujumiwa katika biashara ya Dhahabu nchini Kenya na Uganda.


Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Biteko / Bashunwa/ Kabudi/ mtumieni balozi Mtonga.. Fursa Adhimu ya Kuuza Dhahabu zetu kwa Hawa wachamungu.

    Uhusianno wetu ni Mzuri katika nyanja zote. Ziara ya Mstaafu Dkt Shein ilifana sana.

    Ningependa kipenzi chetu JPJM Amtume as sppecial envoy baada ya Mawaziri kuifanyia kazi hii business oppurtunity ambayo imejitokeza.

    Hapa kazi kwenda mbelee.
    Niko tayari kushiriki kikamilifu katika ujumbe wa kibiashara kutafuta masoko ya Mifugo na Magogo ya Miti na Watalii.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad