Uchaguzi nafasi ya Mwenyekiti na Makamu wake wagonga Mwamba Mjini Babati



Na John Walter-Babati
Zoezi la kupiga kura kumchagua Mwenyekiti na Makamu wake katika Halmashauri ya mji wa Babati limegonga mwamba baada ya wagombea  nafasi hiyo kura zao kulingana mara tatu.

Wapiga kura 12 leo novemba 24,2020  walilazimika kurudia kupiga kura mara zote hizo bila mafanikio hatua ambayo imepelekea kusitishwa zoezi hilo kwa sasa.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mjini Babati Feisal Hamadi amesema kwa sasa wanasubiri uamuzi kutoka ngazi ya juu ya chama.

Wagombea nafasi ya Mwenyekiti ni Yona Wawo diwani wa Kata ya Mutuka ambaye alikalia kiti cha uenyekiti muhula uliopita akichuana na Abarahamani Kololi wa Kata ya Maisaka.

Mgombea wa tatu kutoka kata ya Bagara Yona Sulle alijiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho.

Wagombea nafasi ya Makamu nmwenyekiti ni Hiiti Qambalali Mutlo kutoka kata ya Bonga na Samweli Baran kutoka kata ya Nangara.

Akifungua mkutano huo uliofanyika  katika ofisi za chama hicho Mjini Babati, Mwenyekiti wa  CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Babati Mjini Elizabeth Malle amewataka madiwani wa chama ambao wanaendeleza makundi yasio na tija ndani ya chama kuacha vitendo hivyo badala yake waungane pamoja ili kusimamia miradi ya maendeleo inayoletwa na serikali kwenye maeneo yao.

Alisema kuwa na makundi ndani ya chama ni hatari kwa kuwa  makundi yanakichafua chama ikiwa ni pamoja na kuzorotesha jitahada za chama hicho katika kutekeleza ilani ya uchaguzi pamoja na miradi ya maendeleo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad