Unaambiwa Shamsa Ford Hataki Kuisikia ndoa "Nakula Ujana Kwanza"



STAA wa filamu Bongo, Shamsa Ford amesema kuwa ana muda mrefu wa kula ujana bila kuwa na mwanaume yeyote wa kuishi naye ndani mpaka atakapoona ametosheka vilivyo ndipo atafikiria jambo hilo.


Akizungumza na RISASI JUMAMOSI, Shamsa amesema kuna wakati wanawake wanakuwa hawajamaliza kula ujana wao vizuri na badala yake wakiingia kwenye ndoa moja haikai wala mbili haikai na mwisho wa siku ndoa inavunjika hivyo ni bora kumaliza ujana kwanza.


“Wanawake wengi hawajui, wanakimbilia kuingia kwenye ndoa mapema lakini baada ya muda ndoa inakufa maana bado wanatamani sana mambo ya nje na hata mimi nimejifunza sasa nakula ujana kwanza mpaka nitosheke baada ya miaka kumi mbele ndio nitaingia tena kwenye ndoa rasmi,” alisema Shamsa ambaye aliingia kwenye ndoa miaka kadhaa iliyopita na Rashid Said ‘Chid Mapenzi’ kisha kuachana

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad