Nchini Kenya umefanyika upasuaji wa kwanza wa ubongo huku mgonjwa akiwa macho.
Upasuaji huo umefanyika katika Hospitali ya-Nairobi Hospital, mjini Nairobi Kenya ambapo mgonjwa huyo alikuwa macho na kuweza kuzungumza wakati wote wa upasuaji huo.
Madaktari wa upasuaji wanategemea mchakato wa kipekee a upasuaji unaomfanya mgonjwa awe macho, ambao bado ni hatari, lakini unaweza kuleta matokeo bora na kupunguza hatari ya jeraha katika ubongo.
Katika aina hii ya tiba, madaktari bingwa wa upasuaji wa fuvu la kichwa wanaweza pia kufuatilia hali ya mgonjwa wakati wa upasuaji, hii ikimaanisha kuwa wanaweza kuondoa uvimbe ambao kwa kawaida usingeweza kutolewa salama.
Upasuaji huo wa kufungua fuvu la kichwa au brain craniotomy, kwa lugha ya kitaalamu unaangaliwa kama mafanikio makubwa katika sekta ya tiba kuweza kufanyika nchini Kenya.