Utata kuhusu matokeo ya uchaguzi Marekani



Afisa mmoja utawala aliyekagua matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba 3 nchini Marekani, ametangaza kuwa zoezi la upigaji kura liliendeshwa bila matatizo yoyote ya ukiukaji sheria.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na timu ya kudhibiti miundo ya kiusalama mitandaoni nchini Marekani, iliarifiwa kuwa harakati za uchaguzi huo zilifuatiliwa na kukaguliwa. 


Maafisa waliohusika na ukaguzi walisisitiza kuwa matokeo ya uchaguzi yalikuwa salama na wala hakukuwa na harakati zozote za uvıjaji wa data au zilizotishia kuvuruga takwimu za uchaguzi. 


Maelezo hayo pia yaligusia madai ya wizi wa kura yaliyowasilishwa na Donald Trump kwa kusema, 


"Uchaguzi wa Novemba 3 ulifanya kwa usalama na haki Marekani. Kwa sasa wasimamizi wote wa uchaguzi wanakagua mchakato mzima ilikuhakikisha endapo matatizo yoyote kwa mara ya pili." 


Kwa mujibu wa matokeo rasmi ya uchaguzi , Joe Biden wa chama cha Democrats ndiye mshindi wa kiti cha urais Marekani. 


Kwa upande mwingine, Rais wa sasa na mgombea wa chama cha Republicans  Donald Trump, amekuwa akishutumu chama cha Democrats kwa madai ya wizi wa kura hasa zilizotumwa kwa posta katika majimbo muhimu kama vile Pennsylvania, Arizona na Georgia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad