Vatican Yachunguza Picha ya Mlimbwende wa Brazil iliyopendwa na Papa Instagram

 


Vatican imesema inafanya uchunguzi baada ya akaunti ya Instagram ya Papa kuzua mjadala mara baada ya kupenda picha ya mlimbwende wa Brazil ambaye alikuwa hajavaa nguo ya staha.

Haijawekwa wazi ni lini akaunti hiyo ilipenda picha hiyo ya mlimbwende Natalia Garibotto, ambaye alikuwa amevaa sare ya shule.

Vyombo vya habari vilianza kuripoti kuhusu taarifa hiyo Ijumaa iliyopita , kabla ya kuondolewa kwa alama ya kupendwa kwa picha hiyo.

Maofisa wa baba mtakatifu wameripotiwa kufanya uchunguzi wa jinsi akaunti hiyo ilivyopelekea kupenda picha hiyo.


"Hatuwezi kusema kuwa ni Baba Mtakatifu ndio aliyebonyeza kitufe cha kupenda picha ile, na inabidi tupate ufafanuzi kutoka Instagram ,"alisema msemaji wa Vatican.

Akaunti ya Instagram ya Papa ambayo ina jina la franciscus, ina wafuasi milioni 7.4 kutoka duniani kote.

Vyanzo vya karibu na habari za Vatican, vimesema akaunti hiyo ina inaongozwa na kikosi cha wafanyakazi na uchunguzi wa ndani unaendelea.


Mlimbwende huyo bi Garibotto - aliandika kwenye tweeter "Afadhali nitaenda mbinguni."



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad