Viongozi 20 Chadema Wakamatwa Singida..Mkasa Mzima Huu Hapa

 


VIONGOZI 20 wa Chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema) wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida na kufikishwa mahakamani kwa madai ya kufanya vitendo vinavyochochea uvunjifu wa amani nchini ikiwa ni siku chache baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

 

Mahakama imesema washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka tatu ambapo shitaka la kwanza likiwa ni kuongoza genge la wahalifu, shitaka la pili ni kula njama na la tatu ni kufanya mikusanyiko bila kibali.

 

Wakati huohuo watu saba wakiwemo viongozi wakuu wa chama hicho wakiwa wameshikiliwa na polisi jijini Dar es Salaam baada ya kutangaza kupanga maandamano ya amani siku ya Jumatatu ili kuonyesha kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi.

 

Polisi walisema wamemkamata Mwenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini, Freeman Mbowe, pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam, Boniface Jacob.

 

Aidha, aliyekuwa mgombea nafasi ya urais kupitia chama hicho, Tundu Lissu, alikamatwa jana na kuachiwa muda mfupi baada ya kuhojiwa na jeshi hilo.


 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad