Kituo cha kuhesabu kura kaunti ya Maricopa huko Arizona, kimejipata kikiwa na wakati mgumu wa kufanya maamuzi ya kusitisha shughuli zake baada ya kundi la wafuasi wa Republican kukusanyika nje - wakijibu madai ya mitandao wa kijamii kuwa kura ambazo zinasemekana kuwa za Trump hazitahesabiwa.
Baadhi ya waandamanaji waliingia ndani ya kituo hicho wakisindikizwa na maafisa wa usalama.
Asilimia 82 ya kura katika kaunti ya Maricopa zimehesabiwa huku Joe Biden akiongoza.
Hata hivyo, maafisa wanasema wanazaidi ya masanduku 400,000 ya kura ambazo bado hazijahesabiwa.
Kaunti hiyo ambayo inajumuisha eneo la Phoenix, kwa muda mrefu limekuwa likichukuliwa kuwa ngome ya Republican.