Wanaigeria Wachota Milioni Saba Simba SC




WAKATI Simba ikiwa imeondoka jana jioni kuelekea Nigeria, uongozi wa timu hiyo umebainisha umepata wakati mgumu wa kupata vibali vya kuingia kwenye nchi hiyo ‘visa’ kutokana na kupanda bei ghafla.

 

Simba imeelekea katika nchi hiyo kwa ajili ya mchezo wao wa awali katika ligi ya mabingwa dhidi ya Plateu United ambao unatarajiwa kupigwa wikiendi hii nchini Nigeria. Msafara wa Simba umeondoka na jumla ya wachezaji 25 pamoja na watu wa saba wa benchi la ufundi akiwemo mpiga picha wa timu huyo.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, mratibu wa timu hiyo ambaye yeye ametangulia nchini Nigeria, Abass Ally alisema kuwa changamoto kubwa ambayo wameipata ni gharama za vibali vya kuingia katika nchi hiyo kutokana na bei yake kuwa kubwa tofauti na matarajio.

 

“Huku kila kitu kinaenda vizuri, nategemea kuipokea timu kesho kwa sababu wakitoka huko wanapumzika Ethiopia ambapo watalala halafu ndiyo wataanza safari ya kuja huko kutokea hapo.

 

“Kuhusu mazingira naona yapo sawa kwa sababu huku tutakuwa ugenini, ingawa changamoto kubwa ilikuwa katika suala la visa ambazo tumezipata kwa jumla ya kama milioni saba hivi zote ambazo ni ghali sana tofauti na matarajio. “Jambo lingine ni umbali wa kutoka Lagos hadi kufika Josh ambapo mchezo wenyewe utachezwa,” alisema Ally.

HABARI Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad