Wanajihad 'wawakata vichwa watu 50' Msumbiji



Takriban watu 50 wamekatwa vichwa na wapiganaji wa Kiislamu nchini Msumbiji, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti

Wapiganaji hao waliugeuza uwanja wa kuchezea kandanda kuwa 'kichinjio' , ambapo walikatakata miili ripoti nyengine zinasema

Watu kadhaa pia walikatwa vichwa katika kijiji chengine , vyombo vingine vya habari viliripoti

Uchinjaji huo ndio tukio la hivi karibuni katika msururu wa mashambulizi ya kutisha ambayo yametekelezwa na wapiganaji hao katika eneo lenye utajiri mkubwa wa gesi la mkoa wa Cabo - Delgado tangu 2017.

Hadi takriban watu 2000 wameuawa na takriban 430,000 wengine wamewachwa bila makao katika mzozo huo katika mkoa huo ulio na Waislamu wengi.

Wapiganaji hao wanahusishwa na kundi la Islamic State , ambalo limeingia kusini mwa Afrika. Kundi hilo limetumia sababu ya umasikini na ukosefu wa ajira kuwasajili vijana wengi katika vita vyao vya kutaka kuwa na utawala wa Kiislamu katika eneo hilo.

Wakaazi wengi wanalalama kwamba wamefaidika kidogo na madini pamoja na viwanda vya gesi vilivyopo katika eneo hilo.

Mwandishi wa BBC Jose Tembe kutoka Maputo anasema kwamba mashambulizi hayo ya hivi karibuni ndio yaliokuwa mabaya zaidi kutekelezwa na wapiganaji hao

Watu wengi wameshangazwa na sasa wametoa wito ya makubaliano ya amani kuhusu mzozo huo, anaongezea

Wapiganaji hao walisema 'Allahu Akbar' , [Mungu ni Mkubwa} , wakafyatua risasi na kuchoma baadhi ya nyumba wakati walipovamia kijiji cha Nanjaba usiku wa Ijumaa , kilisema chombo cha habari kinachomilikiwa na serikali cha Mozambique News Agency kikiwanukuu manusura wakisema.

Watu wawili walichinjwa katika kijiji hicho huku wanawake kadhaa wakitekwa , kilisema chombo hicho cha habari

Kundi jingine la wapiganaji lilitekeleza shambulio jingine katika kijiji cha Muatide, ambapo waliwakata vichwa zaidi ya watu 50 , kulingana na chombo hicho cha habari.

Wanakijiji waliojaribu kutoroka walikamatwa na kupelekwa katika uwanja wa kuchezea soka ambapo walikatwa vichwa na miili yao kukatwa katwa vipande vipande katika mauaji yalioanza Ijumaa usiku hadi Jumapili , kilisema chombo cha habari cha kibinafsi The Pinnacle News.

Serikali ya Msumbiji imeomba usaidizi wa kimataifa ili kusaidia kukabiliana na mashambuliaji ya wanamgambo , ikisema kwamba wanajeshi wake wanahitaji mafunzo maalum

Mwezi Aprili , zaidi ya watu 50 walichinjwa na wengine kupigwa risasi katika shambulio la kijiji kimoja katika mkoa wa Cabo Delgabo mapema mwezi huu , watu wengine tisa walikatwa vichwa katika mkoa huohuo.

Makundi ya haki za kibinadamu pia yanasema kwamba wanajeshi wa Msumbiji pia wamedaiwa kutekeleza unyanyasaji wa kibinadamu , ikiwemo kuwakamata watu kiholela mateso na mauaji wakati wa operesheni za kukabiliana na wapiganaji hao.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ponda yuko wapi..??

    Amemuona aliye kwea Pipa..?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad