Wanariadha wa Kenya washinda marathon ya Istanbul



Wanariadha wa Kenya wameshinda mashindano ya mbio za masafa marefu yaliyoandaliwa kwa mara 42 mjini Istanbul nchini Uturuki. 


Benard Cheruiyot Sang alishinda mbio hizo kwa upande wa wanaume, na Diana Chemtai Kipyogei akashinda kwa upande wa wanawake. 


Mwanariadha Sang anayeishi Uturuki na kuiwakilisha nchi hiyo, alimaliza mbio hizo za pikee zinazounganisha mabara mawili. 


Mwanariadha huyo Mkenya alimaliza wa kwanza mbio za masafa ya kilomita 42  na mita 195 ndani ya muda wa 2.11.49.


Muda huo umekuwa bora zaidi kwa Sang katika rekodi yake ya mashindano ya marathon. 


Mshindi wa pili wa mbio hizo alikuwa bingwa wa marathon wa mwaka 2018 Mkenya Felix Kimutai aliyemaliza kwa muda 2.12.00 huku akifuatia na mwanariadha wa Ethiopia Zewudu Hailu Bekele aliyemaliza wa watatu kwa muda wa 2.12.23. 


Na katika upande wa wanawake, MKenya Diana Chemtai Kipyogei alimaliza wa kwanza kwa muda wa 2.22.06.


Mshindi wa pili alikuwa Hiwot Gebrekidan wa Ethiopia aliyemaliza kwa muda wa 2.24.30 huku raia mwenzie Tigist Memuye akimaliza wa tatu kwa muda wa 2.37.52.


Na katika matokeo ya kiujumla kwa wanariadha wa Kituruki, Yavuz Ağralı alimaliza nafasi ya 7 kwa muda wa 2.19.23.


Üzeyir Söylenmez alimfuata kwa muda wa 2.20.34 na Halil Yaşin aliyemaliza kwa muda wa 2.23.09.


Na kwa upande wa wanawake, Tubay Erdal aliyeshika nafasi ya 6 alimaliza kwa muda wa 2.41.11. 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad