Washauri wa Joe Biden wataka hatua za haraka vita ya corona

 


Washauri wa Rais Mteule wa Marekani, Joe Biden wametaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kudhibiti janga la Corona virus wakati maambukizi nchini humo yakifikia Milioni 11.


Wameonya kuwa ucheleweshwaji wa kubadilishana madaraka unaofanywa na Rais Donald Trump unaweza kuathiri zaidi vita dhidi ya Ugonjwa huo ikiwemo mipango ya mgawanyo wa Chanjo.


Ongezeko la visa na vifo limeripotiwa kwenye Miji mbalimbali nchini humo na baadhi ya Miji imetangaza hatua mbalimbali kama kuweka utaratibu wa kuvaa barakoa na kudhibiti idadi ya watu kwenye mikusanyiko.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad