Wana wawili wa kiume wa Rais Donald Trump wamewashutumu wanachama wa Republican kwa kutomuunga mkono rais anapokabiliwa na ushindani mkali kutetea mhula wa pili madarakani.
Donald Trump Jr., speaks as he tapes his speech for the first day of the Republican National Convention from the Andrew W. Mellon Auditorium in Washington, Monday, Aug. 24, 2020. (AP Photo/Susan Walsh)
Mwana mkubwa wa bwana Trump Don Jr alikosoa chama kwa kuwa “dhaifu”. Ndugu yake Eric alionya: “Wapiga kura wetu hawatawahi kuwasahau mkijifanya wanyonge!”
Hatua hiyo inaasharia ya mgawanyiko ulioibuka kati ya washirika wa Trump ndani ya chama.
Ushandani mkali umeshuhudiwa lakini mgombea wa Democratic Joe Biden anyone kana kuelekea kupaya ushindi.
Bwana Trump ameapa kupinga matokeo ya uchaguzi huo mahakamani akitilia shaka shughuli ya kuhesabu kura inavyoendeshwa akidai kumekuwa na visa vingi vya udanganyifu.
Wanasiasa wa ngazi ya juu katika chama cha Republican kama vile seneta wa Utah Mitt Romney na Gavana wa Maryland Larry Hogan wameonya hatua ya kuhujumu mchakato wa kidemokrasia.
Lakini Don Jr, ambaye anaaminiwa kuwa na ndoto ya kujiunga na siasa ameelekeza ghadhabu yake kwa wale walio na azma ya kuwania urais mwaka 2024.
Aliandika kwenye Twitter: “Hatua ya kutochukua hatua kwa wanasiasa ‘wanaotaka tiketi ya 2024 ya [Republican] ‘ inashangaza sana .
“Wana nafasi ya kuonesha kutoridhishwa kwao na hali ilivyo na kupigania wanachokiamini lakini wanahofia kuangaziwa vibaya na vyombo vya habari. Msiwe na hofi @realDonaldTrump ataendelea kupambana na wao wakiangalia!”
Ujumbe huo wa Twitter hiyo ulikuwa unamjibu Mike Cernovich, mwanaharakati wa masuala ya wanaume na mfuasi wa Trumpr, ambaye alikuwa amemkosoa mjumbe maalum wa zamani wa rais katika Umoja wa Mataifa , Nikki Haley.
Anadhaniwa na wengi kwamba anapania kuingia Ikulu ya White House mwaka 2024.
Bwana Trump Jr aliendelea kuandika: “Republicans wamekuwa wanyonge kwa miongo kadhaa hali iliyotoa nafasi kwa wapinzani kufanya vitu hivi.”
Ndugu yake Eric, aliandika: “Sisi ni Warepublican! Tuna ubavu wa kukabiliana na udanganyifu. Wapiga kura wetu hawatawahi kusahau mlichokifanya!”
Section divider
Ndugu hao wawili waliendelea mbele na kuwataja na kuwasifu wanacham wa Republican ambao wamejitokeza kumuunga mkono baba yao.
Wafuasi wengine wa Trump walimlenga moja kwa moja Haley. Matt Gaetz, mbunge wa Florida, aliandika : “Wakati baahi yetu tunampigania Rais Trump… Nikki Haley anamuomboleza. inasikitisha!”
Katika miaka yake minne ya siasa, bwana Trump amefanikiwa kutumiachama cha Republican kwa maslahi yake na kupata uungwaji mkono wa 90% kutoka kwa wanachama wa dhati wa chama.
Wafuasi wengine wa Trump walimlenga moja kwa moja Haley. Matt Gaetz, mbunge wa Florida, aliandika : “Wakati baahi yetu tunampigania Rais Trump… Nikki Haley anamuomboleza. inasikitisha!”
Katika miaka yake minne ya siasa, bwana Trump amefanikiwa kutumiachama cha Republican kwa maslahi yake na kupata uungwaji mkono wa 90% kutoka kwa wanachama wa dhati wa chama.
Ilani ya chama mwaka huu ilifutwa na kubadilishwa na ahadi ya “kuunga mkono ajenda ya kwanza ya rais Marekani”.
Mzozo kati ya familia ya Trump na usimamizi wa chama huenda ukaibua maswali kuhusu mkondo utakaochukuliwa n chama hicho baa ya Trump kuondoka, iwe ni mwaka 2020 au 2024.