Watu 3 wameuawa kwa kushambuliwa na Tembo huku 1 akijeruhiwa katika vijiji vya Mindu na Tulieni Wilayani Tunduru
Afisa Wanyamapori wa Wilaya, Ally Mbega Ally amesema waliofariki ni Jamili Mchopa (47), Justine Mchopa(54) na Stephano Joseph(78)
Marehemu waliwazingira Tembo wakati wakinywa maji katika Bwawa lililopo kijijini hapo. Aliyejeruhiwa ametambulika kwa jina moja la Zuberi