Watu 30 wafariki kwa ugonjwa usiojulikana nchini Nigeria



Watu 30 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kushangaza usiojulikana uliozuka wiki moja katika mkoa wa Delta nchini Nigeria.


Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya kitaifa, iliarifiwa kuwa ugonjwa huo usiojulikana ulisababisha watu 30 kufariki katika maeneo ya Ute Okpu na Idumusa ndani ya wiki moja.


Viongozi wa mkoa huo pia walitoa maelezo na kubainisha kwamba watu waliofariki walikuwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 18-25. 


Viongozi waliongezea kusema kuwa utafiti unaendelea ili kugundua chanzo halisi cha vifo huku wakifahamisha kwamba kabla ya kufariki, watu hao walionyesha dalili za kutapika damu, udhaifu wa hali, maumivu ya mwilii na kichwa. 


Miezi 5 iliyopita, watu wapatao 1000 pia walipoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kushangaza usiojulikana nchini humo. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad