Watu 5 wauawa, 40 wachukuliwa mateka kwenye mashambulizi ya msikiti nchini Nigeria





Kundi la watu waliojihami kwa silaha limeripotiwa kushambulia msikiti mmoja ulioko mkoani Zamfara nchini Nigeria na kuwaua watu 5 na kuwachukuwa mateka watu wengine 40.
Washambuliaji hao wengi wasiojulikana walivamia msikiti huo kwa kutumia pikipiki.

Vikosi vya usalama viliwasili katika eneo la tukio na kuanzisha uchunguzi juu ya mashambulizi hayo.

Kwa kipindi cha miaka 4, mkoa wa Zamfara umekuwa ukikumbwa na visa vya migogoro ya kikabila kati ya wafugaji na wakulima wa jamii ya Fulani.

Jamii ya Fulani inayohusika na ufugaji, imekuwa ikihamia vijiji mbalimbali vya maeneo ya kusini mwa nchi na mara kwa mara wamekuwa wakishambulia wakulima na kuwaibia mifugo yao.   

Makundi mengi ya silaha yamekuwa yakitumia kigezo hiki kuendesha mashambulizi.

Watu wapatao 2,000 wamepoteza maisha na wengine maelfu kulazimika kuhama makazi yao kutokana na migogoro katika eneo hilo.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad