Wema Sepetu na Kiu ya Kupata Mtoto "Nikipata Mtoto Lazima Nichanganyikiwe Kwanza"

 

 

Mrembo Nyota anayesukuma maisha yake kupitia ulimwengu wa Bongo Movie, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amevunja ukimya na kusema kuwa siku Mungu akimjalia kupata mtoto wake lazima achanganyikiwe kwanza.


@wemasepetu ambaye kwa sasa anatamba na kipindi chake cha mapishi cha Cook With Wema Sepetu, ameeleza hilo kwenye Insta story yake baada ya kutoa nafasi ya kuulizwa maswali na mashabiki wake ambapo moja ya swali lilikuwa ni siku akipata mtoto itakuwaje ambapo alijibu hivi:


“Nikipata mtoto wangu naweza nikachanganyikiwa siku mbili au tatu naamini, hata mimi ningependelea hivyo ipo siku inshaallah” alijibu Wema. Hata hivyo kuhusiana na kumualika Zari kwenye kipindi chake, Wema amesema kuwa kama Zari akiridhia, anaweza kumualika kwani yeye hana tatizo naye.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad