WHO: Ebola imekwisha DRC

 


Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema kuwa sasa nchi hiyo imeondokana na ugonjwa wa Ebola baada ya siku zaidi ya 40 bila kuripotiwa kwa ugonjwa huo.

Mlipuko wa hivi karibuni kaskazini magharibi mwa nchi hiyo ulikuwa wa tatu katika kipindi cha miaka miwili.


Lakini chanjo na tiba zilizobuniwa wakati wa majanga yaliyotangulia sasa hivi zinatoa matumaini kwa wagonjwa.


Tangu mwaka 2018, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekabiliwa na milipuko ya ugonjwa wa Ebola kufuatana.


Mwanzoni mwa Juni wagonjwa kadhaa walipatikana na ugonjwa huo katika mwa eneo la Mbandaka.


Watu 130 waliambukizwa ugonjwa huo huku 55 kati yao walifariki dunia.


Visa vya ugonjwa huo eneo la Mbandaka vilibainika wakati mlipuko wa Ebola mashariki mwa nchi hiyo unakaribia kufikia ukomo wake.


Zaidi ya watu 2,000 wamekufa kutokana na ugonjwa huo katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri kwa zaidi ya miaka miwili.


Huo ulikuwa mlipuko wa pili mkubwa zaidi duniani.


Shirika la Afya Duniani limeidhinisha chanjo iliyotolewa na kampuni ya dawa ya Merk ambayo imetolewa kwa watu 400,000 kote nchini humo.


Mwezi uliopita, Shirika la Dawa nchini Marekani limeidhinisha dawa ya Inmazeb kama tiba ya Ebola, baada ya kufanyiwa majaribio huko Congo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad