WHO: Maambukizi yapungua Ulaya





Shirika la Afya duniani WHO limesema kasi ya janga la virusi vya corona imepungua mnamo juma lililopita, lakini viwango vya vifo vimeongezeka. 
Hayo yanaarifiwa kukiwa na jumla ya vifo vipya 67,000 vilivyoripotiwa. Shirika hilo lenye dhamana ya afya duniani limesema pamoja na kasi kupungua lakini viwango vya visa vya maambukizi barani Ulaya pamoja na idadi ya vifo bado vipo juu. 

Kwa Afrika shirika hilo lilizingatia maeneo ya ongezeko la maambukizi na vifo katika mataifa ya Afrika Kusini, Algeria na Kenya. 

WHO imesema kwa juma lililopita Ulaya kuliripotiwa kupungua kwa asilimia 6, kutoka 10 ya wiki nyingine kabla ya hiyo, hatua ambayo masharti ya kujilinda yaliyowekwa katika eneo zima la bara hilo yamesaidia kupunguza kuenea kwa virusi hivyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad