Yanga Ina Balaa, Yatibua Rekodi ya Biashara United Baada ya Dakika 248

 


USHINDI wa bao 1-0 walioupata Yanga jana Oktoba 31 dhidi ya Biashara United Uwanja wa Karume umetibua rekodi ya kikosi cha wanajeshi hao wa mpakani kucheza ndani ya dakika 180 bila kupoteza mbele ya Yanga kwenye mechi walizokutana kwenye uwanja wao wa nyumbani.


Kwa msimu wa 2018/19 Yanga ilipokutana na Biashara United ililala kwa bao 1-0 na msimu wa 2019/20 Yanga iliporejea tena Karume ilikutana na kisiki baada ya kugawana pointi mojamoja kwenye sare ya bila kufungana.

Baada ya dakika 180 za nyuma kumeguka ngoma imekuja kutibuliwa baada ya dakika 248 kwa kuwa Yanga ilifunga bao jana dakika ya 68 kupitia kwa Michael Sarpong ambaye kwa sasa ana mabao mawili ndani ya Ligi Kuu Bara.

Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa ni jitihada za wachezaji wake katika kusaka matokeo ndani ya uwanja anaamini kwamba watazidi kufanya vizuri kwenye mechi zao zijazo.

"Ni jitihada za wachezaji ndani ya uwanja, bado nina amini kwamba watafanya vizuri kwenye mechi zijazo hivyo kikubwa kwa mashabiki ni kuendelea kutoa sapoti."

Yanga ikiwa nafasi ya pili inashikilia rekodi ya kuwa timu yenye safu kali ya ulinzi ikiwa imeruhusu mabao mawili ndani ya mechi nane ambazo imecheza mpaka sasa.

Mwadui FC ni namba moja kwenye kuruhusu mabao ambapo ikiwa imecheza mechi 9 imeruhusu mabao 19.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad