Yanga SC Wafungukia Mwamnyeto, Fei Toto Kwenda TP Mazembe



BAADA ya tetesi kuzagaa za kiungo fundi wa Yanga, Feisal Salum na beki wa kati wa timu hiyo, Bakari Mwamnyeto kuhitajika na Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, bosi mkubwa wa timu hiyo ameibuka na kufungukia dili hilo.


Hivi karibuni kuliibuka tetesi hizo za nyota hao tegemeo kwenye kikosi cha Yanga kuhitajika na klabu hiyo kubwa na kongwe yenye rekodi ya kubeba mataji ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Imeelezwa kuwa, wachezaji hao wanahitajika kwa ajili ya kusajiliwa moja kwa moja na siyo kwa ajili ya majaribio baada ya kuona uwezo wa kila mmoja wakiwa na Yanga.


Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alisema kuwa bado hawajapokea taarifa rasmi za kiofisi kutoka Mazembe, zaidi wanasikia tetesi pekee.


Aliongeza kuwa, wao kama uongozi hawatamzuia mchezaji yeyote kuuzwa nje ya nchi, kikubwa watakachokiangalia ni maslahi ya klabu na mchezaji mwenyewe.


“Kama uongozi hatushangai kusikia taarifa za wachezaji wetu Mwamnyeto na Fei Toto kuhitajika Mazembe, lipo wazi ni kati ya wachezaji waliokuwepo kwenye viwango vikubwa katika timu yetu.

“Siyo hao pekee, pia wapo wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa wa kucheza soka nje ya nchi na hiyo ni kutokana na usajili bora tulioufanya Yanga katika msimu huu.

“Hivyo kama uongozi kwetu ni ngumu kumzuia mchezaji kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi, kwani soka ndiyo maisha na kikubwa hizo timu zifuate sheria za usajili kwa klabu husika inayommiliki mchezaji,” alisema Mwakalebela

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad