Mechi ya Kariakoo Derby ambayo ni ya ligi kuu bara, kati ya Yanga dhidi ya Simba imemalizika leo jioni Novemba 7, kwenye dimba la Mkapa kwa sare ya 1-1 mechi ambayo imewafanya mashabiki kupokezana kushangilia, wana Jangwani wakicheza kipindi cha kwanza na Mnyama kipindi cha pili.
Yanga walianza vizuri kipindi cha kwanza na Kocha Kaze alifanikiwa na mpango mkakati wa kuwasubiri Simba na kutumia mashambulizi ya kushtukiza, mashambulizi yaliwapa wakati mgumu mabeki wa kati wa Simba,
Mashambulizi hayo yalifanikiwa kupata bao kwa mkwaju wa penati iliwekwa wavuni na mshambuliaji Michael Sarpong, baada ya mlinzi wa kimataifa wa Kenya Joash Onyango kucheza faulo ambayo mwamuzi wa kati aliamuru kuwa penati
Kipndi cha pili Simba walionekana kubadilika na kuanza kushambulia kwa kasi tofauti na kipindi cha kwanza ambapo walionekana kutengeneza mashambulizi yao kwa taratibu na kuingia kwa Hassan Dilunga kuliifanya Simba kucheza kwa kasi.
Wakati mashabiki wengi wakiamini kuwa mechi inaisha kwa sare, Simba walisawazisha kupitia kwa Joash Onyango kwa kichwa akiunganisha kona Luis Miquissone na kufanya matokeo kuwa 1-1.
Kwa matokeo ya leo Yanga amefikisha pointi 24 nyuma kwa pointi moja kwa vinara Azam fc wenye pointi 25, wekundu wa msimbazi wanaendelea kushika nafasi ya tatu kwa alama 20.