JUMAMOSI ijayo ni siku ya mechi kali yenye historia kwenye soka la Bongo ambapo mabingwa watetezi Simba watavaana na mabingwa wa kihistoria Yanga.Hii itakuwa mechi ya kwanza kwa timu hizo kukutana msimu huu ambapo Simba wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 16 baada ya kufanikiwa kucheza michezo nane huku Yanga wakiwa nafasi ya pili baada ya kukusanya pointi 22 baada ya kucheza michezo nane.
Katika mchezo wa Jumamosi, Simba ndiyo wanaonekana kuwa kwenye presha kubwa zaidi kutokana na matokeo ambayo wameyapata siku chache zilizopita baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo dhidi ya Prisons walipochapwa bao 1-0 na dhidi ya Ruvu Shooting walipolala kwa bao 1-0.
Hali hii inaonyesha dhahiri kuwa kama Simba watapoteza mchezo ujao dhidi ya Yanga basi mambo yao yanaweza kuwa magumu zaidi kwa kuwa Yanga watakuwa wamewaacha kwa pointi 11 baada ya michezo tisa tu na mambo yanaweza kuwa magumu kwao.
Lakini pia Simba wapo kwenye presha kubwa baada ya kuonekana kuwa na wachezaji muhimu wenye majeraha tofauti na watani wao.
Simba inatajwa kuwa itamkosa Chris Mugalu na Meddie Kagere na hawa wameonekana kuwa nguzo muhimu sana kwao,wanachosubiri kwa sasa ni kuhakikisha wanamlinda staa wao John Bocco awe fiti kwa asilimia 100 kabla ya mchezo huo.
Hali hii imewafanya Simba wapangue kikosi chao na wanaonekana kuwa wana pigo kubwa kwao tofauti na Yanga ambao wanaonekana kuwa imara kwa asilimia 100, huku wakimkosa kiungo wao Carlos Carlinhos ambaye bado hawana uhakika asilimia zote kama atakosa Said ally,Dar es SalaamKocha Simba SC aanza na Kagera BIG bosi wa benchi la ufundi la Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck amefunguka kwamba anaanza maandalizi ya kushinda kwenye mchezo wao wa dabi dhidi ya Yanga kwa kuwapa kipigo Kagera Sugar leo Jumatano.
Kocha huyo ameongeza kuwa huo ni mpango wake wa kuhakikisha hapotezi pointi yoyote kwenye mechi zao hizo mbili licha ya kuwa na ugumu mkubwa.Sven leo Jumatano ataiongoza Simba kupambana na Kagera Sugar kwenye mechi itakayopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar.
Kikosi hicho Jumamosi hii kitacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.Mbelgiji huyo ameliambia Championi Jumatano, kuwa mechi hizo ni ngumu kwao lakini watapambana kushinda zote kutokana na mkakati wa kutopoteza pointi ambao wamejiwekea kwa sasa.“
Tunacheza Jumatano (leo) kisha Jumamosi tunacheza tena kwenye mechi kubwa ya dabi. Hizi zote ni mechi muhimu kwetu kwani nataka tushinde na tupate pointi.“
Tuna mkakati wa kutopoteza pointi tuliojiwekea kwa sasa, tutaanza kushinda mbele ya Kagera Sugar kabla ya kumaliza kuchukua pointi kwa Yanga kwenye dabi,” alimaliza Mbelgiji huyo.mchezo huo.Kikosi cha Yanga kinaonekana kuwa bora kwenye mchezo huo tofauti na Simba na inaelezwa kuwa leo kitabadilishwa sehemu mbalimbali ili kuhakikisha Jumamosi kinakuwa kwenye ubora wao.
Kikosi cha Yanga ambacho kinatarajiwa kuanza Jumapili ni Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Mukoko Tonombe, Farid Musa, Feisal Salum, Michael Sarpong, Yacouba Sogne na Tuisila Kisinda.
Huku Simba wao wakitarajiwa kupanga kikosi chao kama ifauatavyo: Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Muhammed Hussein Tshabalala, Pascal Wawa, Joash Onyango, Gerrard Mkude, Luis Miquissone, Mzamiri Yassin, John Bocco, Larry Bwalya na Clotaus Chama.