Yanga Yatangaza Bosi Mpya, Yaanika Sakata la Morrison, Kabwili




 

UONGOZI wa Klabu ya Yanga SC, leo Novemba 20 umemtangaza Hajji Mfikirwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu  mpya ambaye anachukua nafasi ya wakili Simon Patrick ambaye amesimamishwa kazi.

 

Wakili Simon amesimamishwa kazi Novemba 18 kutokana na tuhuma ambazo zinamkabli hali iliyopelekea kuundwa kamati huru kwa ajili ya kuchukunguza suala hilo kabla ya kutolewa hukumu.

 

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Frederick Mwakalebela amesema Kamati ya Utendaji inamuamini Hajji ataweza kuipeleka mbele klabu hiyo kutokana na uwezo mkubwa alio nao.

 

Aidha Mwakalebela ameliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuzifanyia kazi kesi zao walizo ziwasilisha ambazo ni ile ya Ramadhani Kabwili,  pamoja na mkataba wa Bernard Morrison kwa kuwa wanaelekea katika dirisha dogo la usajili.

 

Mwakalebela ameongeza kuwa kama suala la Morrison ambalo limefikishwa Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo ya FIFA (CAS) lisipofanyiwa kazi mpaka dirisha la usajili likafunguliwa huenda mkataba ukabadilishwa kwa kuwa muda utapatikana dirisha likiwa wazi.

 

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad