Z Anto afunguka mapya ya Binti Kiziwi



Msanii Z Anto amesema alikuwa na lengo la kumtengenezea mtaji 'Video Vixen' Binti Kiziwi baada ya kutoka gerezani nchini China ambapo alifungwa kwa miaka kadhaa, ila bahati mbaya alipata washauri wengine ambao walishawishi tofauti na walivyopanga.

Z Anto amesema Binti Kiziwi alikuwa hawezi kusimama mbele ya jamii, aliigopa Serikali na baadhi ya watu pia alikuwa hataki kuonekana kama amerudi baada ya kutoka gerezani kwa sababu alihofia kuingia tena kwenye matatizo.


"Nilikuwa na lengo la kumtengenezea mtaji ili kupambana na maisha yake, wakati nawaza kumsaidia akapata wengine wakamshauri na kumshawishi mwisho wa siku nikaishia hapo, kwa asilimia nyingi alinufaika na mimi kwa sababu alikuwa hawezi kusimama mbele ya jamii, aliiogopa Serikali na baadhi ya watu, nilikuwa naye na nilimtambulisha tena kwa jamii ili aonyeshe kitu anachotaka kukifanya" ameeleza Z Anto 


Binti Kiziwi na Z Anto waliwahi kuwa kwenye mahusiano kipindi cha nyuma baada ya kumaliza kufanya kazi ya pamoja kwenye video ya wimbo wa 'binti kiziwi' ambayo ilitoka mwaka 2008.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad