Ili kuweza kutambua kama umeugua ugonjwa wa kisukari unatakiwa kujua dalili za awali za ugonjwa huo ambazo ni;
1. Kukojoa mara kwa mara.
Ugonjwa wa Kisukari unasababisha sukari kutolewa kwenye njia ya mkojo. Sukari inapotolewa huambatana na maji hivyo kukufanya upate mkojo kila mara.
2. Kuhisi Kiu mara kwa mara.
Unapokuwa na kisukari unapoteza maji mengi kwenye mkojo hali hii husababisha kupata koi mara kwa mara.
3. Kusikia njaa kali kila mara.
Mwili unapoteza uwezo wa kutumia sukari katika kazi zake. Hali hii hufanya mwili wako kuhisi kuwa hakuna chakula cha kutosha. Hii ndio sababu inakufanya kuhisi njaa kila mara na hata baada ya kula unaendelea kuhisi njaa.
4.Uchovu wa mwili
Hii hutokana na mwili kushindwa kutumia sukari kutengeneza nishati ya kuwezesha mwili kufanya kazi zake.
5.Kupoteza uzito/Kukonda
Ugonjwa wa Kisukari hupunguza uwezo wa mwili kuhifadhi sukari kwenye misuli. Hivyo mwili wako utaanza kupoteza uzito na kuanza kukonda.