Zuchu mambo safi, alamba dili lingine




Kampuni ya vipodozi ya Tridea Cosmetics, inayo furaha kumtangaza kuingia makubaliano na msanii Zuhura Othman ‘Zuchu’, kuwa balozi wa bidhaa zake.



Zuchu ambaye ni msanii wa muziki wa bongo fleva katika lebo ya WCB, atakuwa balozi wa bidhaa za Tridea akihusika kwenye matangazo ya TV, magazeti na mitandao ya kijamii.”

Zuchu ni msanii wa kike anayekubalika kwa sasa na atakuwa balozi mzuri kwa wengine kupitia bidhaa zetu ikiwemo kuwasaidia wanawake kutumia na kujisikia vizuri. “Tumeamua kufanya naye kazi baada ya kuona kazi zake zinakubalika na atakuwa balozi mzuri kwa wengine,” alisema Mtendaji Mkuu wa Tridea Cosmetics, Grace Luswaga.

“Bidhaa za Tridea kwa wanawake zinasaidia kuwaweka kwenye mwonekano mzuri na kujisikia huru kila wakati,” alisema.

Akizungumzia hilo, Zuchu alisema kuwa amefurahia kuingia mkataba na Tridea Cosmetics na huo utakua ushindi wa wanawake wote na kina mama wa Tanzania nzima.”Ninafurahia kuingia mkataba na Tridea Cosmetics na kwani nitakua balozi mzuri kwa wanake wenzangu na kina dada, mama yangu pia anatumia bidhaa hizi na mimi tangu nikiwa mdogo nimekuwa nikizitumia,” alisema Zuchu.

Zuchu ni msanii aliyetoka kwenye familia ya muziki ambapo ameshafashirikishwa kwenye wimbo wa Mauzauza na mama yake Khadija Kopa, pia Cheche ya Diamond Platnumz.

Zuchu kwa sasa anafanya vizuri katika muziki wa bongo fleva na kuendelea kuwateka mashabiki kila kona ikiwemo mitandao ya kijamii.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad