Afisa wa uchaguzi wa jimbo la Georgia nchini Marekani amesema Trump anachochea ghasia za uchaguzi

 


Afisa wa uchaguzi wa jimbo la Georgia nchini Marekani amesema Rais Donald Trump atachukua jukumu la ghasia zozote zitakazojitokeza kutokana na madai ya udanganyifu katika uchaguzi ambayo hana uthibitisho


Katika taarifa yake, Gabriel Sterling, kutoka Republican, alisema: "Kila kitu kimeenda mbali sana! Yani kila kitu! Inabidi kuachana na haya mambo!"


Jimbo la Georgia limefanya marudio ya kuhesabu kura kwa mara ya pili baada ya kampeni ya Trump kuomba kura zirudiwe kuhesabiwa.


Rais mteule wa Marekani Joe Biden kutoka chama cha Democratic alitangazwa kuwa na ushindi mdogo katika jimbo hilo.


Msemaji wa kampeni za Trump, Tim Murtaugh alisema anajaribu kuhakiki kuwa kura zote zilihesabiwa na hakuna kura zilizoibiwa.


"Mtu yeyote asijihusishe katika vitisho na ghasia , na kama zimetokea tunalaani vikali vitendo hivyo."


Akizungumza kwa ghadhabu katika mkutano na waandishi wa habari huko Atlanta siku ya Jumanne, bwana Sterling, msimamizi wa mfumo wa upigaji kura aliwakemea wanachama wenzake wa Republicans, pamoja na rais.


Alisema, kwa miaka 20 ambayo amekuwa akisimamia mfumo wa upigaji kura katika uchaguzi wa taifa hilo, nadharia ya kutokubalika kwa ushindi, kumesababisha apate vitisho vya kuuawa na familia za wafanyakazi wamekuwa wakisumbuliwa, aliongeza .


Mwanaume mmoja amekuwa akimtumia vitisho na kushutumiwa kushtakiwa kwa kosa la uhaini , Bwana Sterling alisema,baada ya kupeleka matokeo aliweza kusoma katika katika kompta.


Bw. Sterling alisema yeye mwenyewe wakati polisi akiwa nje ya nyumbani kwake alipata vitisho, huku mke wa katibu wa jimbo la Georgia, Brad Raffensperger, alipata vitisho vya kingono kupitia simu yake".


"Rais hajakemea hili suala wala kuchukua hatua zozote," aliongeza bwana Sterling. "Maseneta, hamjakemea hatua hii wala lugha hii.


Tunahitaji uingilie kati na kama utachukua msimamo wa uongozi, onyesha msimamo wako!"


Aliongeza kusema kuwa : "Vitisho vya kifo, vitisho vya kimwili, na vitisho vingine, vimepita kiasi, sio sawa, wamekosa sababu za kimaadili kudai kile wanachokidai."


Bw Sterling pia alizungumzia kuhusu vitisho vya ghasia dhidi ya Chris Krebs, ambaye alifutwa kazi mwezi uliopiita kama mkuu wa Shirika la miundo mbinu ya usalama wa kimtandao nchini Marekani baada ya kutofautiana na madai ya wizi wa kura ya Bw.Trump.


Bw. Sterling alilaani matamshi ya wakili wa Bw Trump Joe Di Genova, ambaye Jumatatu alisema kuwa Bw Krebs anapaswa "kutolewa nje usiku na kupigwa risasi".


Akimzungumzia Bw Trump moja kwa moja, Bw Sterling aliendelea kusema kuwa : "Una haki ya kwenda mahakamani. Kile ambacho hauna uwezo wa kufanya , na unapaswa kujitokeza na kusema hili, ni kuacha kuwachochea watu kufanya vitendo vinavyoweza kusababisha ghasia.


"Mtu fulani ataumia, mtu fulani atapigwa risasi,mtu fulani atauawa, na sio sahihi."


Aliongeza kuwa: "Kuwa mtu mkubwa hapa, na usitishe haya, ingilia kati, waambie wafuasi wako, msiwe wenye kufanya ghasia,msiwatishe watu. Yote hayo ni makosa, sio umarekani.


Mwanasheria Mkuu wa Marekani apinga madai ya wizi wa kura

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad