Ang’atwa na nyoka zaidi ya mara 200, asimulia maumivu aliyopitia

 


Kila baada ya dakika tano, mtu mmoja duniani hufariki kutokana na kung’atwa na nyoka. Watu wengine wanne hupata ulemavu wa maisha kutokana na kung’atwa na hao nyoka.



A cobra being milked for its poison


Lakini kuna watu ambao huchukua hatari si haba kwa kufanya majaribio ya kung’atwa na reptilia hao hatari.


Tim Friede, ambaye anaishi katika jimbo la Wisconsin, Marekani huchukua picha za filamu wakati akiruhusu kwa makusudi kushambuliwa na nyoka wenye sumu, na huchapisha video hizo kwenye mtandao maarufu wa YouTube.


 Tim Friede huhadithia wafuasi wake YouTube namna gani hujisikia baada ya kung’atwa na nyoka.

Katika moja ya video hizo, anaonekana akiongea mara tu baada ya kung’atwa mara mbili na nyoka hatari aina ya songwe (black mamba), akipuuzilia mbali damu inayomchuruzika mkononi.


“Songwe hukupatia maumivu makali na ya haraka. Ni kama kung’atwa na nyuki elfu moja. Nyuki wanaweza kuwa na miligramu moja ama mbili za sumu, lakini songwe ana miligramu 300 mpaka 500.”


Amefanya mazungumzo na BBC na kueleza kile kilichotokea baada ya hapo: “Napata uvimbe wa mwili baada ya sumu kuingia. Kwa siku chache zinazofuata nakuwa mtu wa kulala tu. Kulingana na jinsi mwili wangu unavyovimba, naweza kukadiria kiasi gani cha sumu kiliniingia kutoka kwa nyoka. Ni maumivu makali sana,”anaeleza huku akionesha kumaanisha anachokisema.


Hatari na haifai

Lakini si kila mtu anavutiwa naye kama kwa wafuasi wake kwenye mtandao wa YouTube.Tim Friede getting bitten by a snake


Tim Friede anaamini mwili wake unaweza kukabiliana na aina yoyote ya sumu ya nyoka

“Hatuna tulijualo kwa yale ambayo watu hawa wanayafanya. Hii ni hatari na haikubaliki. Hatufanyi nao kazi,” anasema Dkt kutoka Chuo cha Matibabu ya Kitropiki cha Liverpool, Uingereza.


Taasisi yake ni miongoni mwa vyuo vinavyofanyia utafiti juu ya kinga ya sumu ya nyoka.


Kwa kawaida, kinga mpya hujaribiwa kwa panya na wanyama wengine wa maabara na ikionekana kuwa inafaa baada ya hapo ndipo huanza kujaribiwa kwa binaadamu tena chini ya uangalizi maalumu.


“Watu hupata kinga binafsi sababu hakuna udhibiti wa kutosha. Lakini vitendo hivyo aghlabu hupelekea vifo. Ni bora mtu kujitenga navyo,” amesisitiza Dkt Ainsworth.


Lakini kwa ujumla wake katika soko la dawa la dunia kumekuwa na ukosefu wa mwongozo wa kufanya utafiti wa kinga dhidi ya sumu ya nyoka.


“Hakuna uzalishaji wa pamoja, viwango vya ubora wala usalama,” inaeleza taasisi ya Wellcome Trust ya Uingereza ambayo inaongoza harakati za kisayansi za kupatikana kwa kinga mpya.


Hatari ya Kifo

Friede hata hivyo anakanusha vikali kuwa anahatarisha maisha yake ili kuongeza ushawishi na ufuasi katika mitandao ya kijamii.


“Sikulenga kutengeneza video za YouTube – Nilitaka kuokoa maisha ya watu na kuleta mabadiliko. Nimetumia mtandao wa YouTube ili kuwapata madaktari ambao nafanya nao kazi ka sasa. Ilikuwa ni mchezo wa kubahatisha, na nikafanikiwa,” amesema.Tim Friede showing one of the snakes he is keeping


Tim Friede anasema alikaribia kufa mara 12 kutokana na mashambulio ya nyoka

Kati ya aina 3,000 za nyoka, ni aina 200 tu ambao wana kiwango cha sumu ambacho kinaweza kumuua ama kumpa ulemavu wa kudumu mwanadamu.


Friede tayari ameshakutana na kushambuliwa na wengi kati ya nyoka hao.


Mpaka sasa ameshang’atwa mara 200 na nyoka aina mbali mbali katika kipindi cha miaka 20.


Pia amejidunga zaidi ya mara 700 sumu ya nyoka.


Kiwango cha sumu hutofautiana baina ya nyoka. Wakati mwengine nyoka anaweza kukung’ata na asitoe sumu.



“Kama hauna kinga ya sumu ya nyoka kama songwe, mara moja mfumo wako wa fahamu huathirika. Mwili wako utazizima na kushindwa kupumua, hutaweza kuongea, kidogo kidogo utapoteza mwelekeo kisha utapooza – sababu mfumo wako wa fahamu utakuwa umeathirika hutafikiria chochote mpaka unafariki,” Friede amesema.


Swila (cobra) huuma zaidi


Friede huwaweka nyoka wenye sumu kwenye uwa wake na huwajaribu sumu yao kwenye mwili wake. “Ninao swila (cobra) maji kutoka Afrika. Akikuuma maumivu yake ni makali. Ilikuwa balaa, niliogopa sana.”


Swila maji wana sumu kali inayoathiri mfumo wa seli za mwili.


Friede anafanyia kazi nadharia kuwa mwili ukiwa unapokea sumu ya nyoka kwa uchache kwa muda mwili huo unaweza kutengeneza kinga ya asili baada ya muda fulani, lakini nadharia hiyo inapingwa vikali.Songwe ama black Mamba


Songwe (black mamba) ni moja ya nyoka hatari zaidi – sumu yake inaweza kumuua binadamu chini ya dakika 30.

Kutengeneza kinga

Nadharia kama hiyo – japo inatumia wanyama – ndiyo ambayo ilifanya kupatikana kwa baadhi dawa za kuzuia athari za sumu ya nyoka tunazozitumia leo.


Mfumo wa utengenezaji wa dawa hizo haujabadilika sana toka karne ya 19, japo leo tupo karne ya 21 na hutumia zaidi wanyama kutengeneza kama kondoo na farasi.


“Kuna hawa viumbe wanataka kuniua, nami sitaki kufa, Hivyo mie huamua kuwa ‘farasi’. Kwanini tusijitengenezee kinga?” anauliza Friede.


Bwana huyo mwenye miaka 51 ambaye alikuwa dereva wa malori ya masafa marefu si mtaalamu wa kinga wa kusomea na wala hajawahi kukanyaga Chuo Kikuu. Ilikuwa ni woga wake wa kung’atwa na nyoka ndiyo ulimsukuma kuanza kufanya majaribio yake hayo miaka 20 iliyopita.


Awalia lianza majaribio yake na nge na buibui na kisha akapanda mpaka kwa nyoka.A snake charmer in Pakistan


Nyoka huogopwa pamoja na jamii nyingi, lakini wengine huwatumia kama sehemu ya utamaduni

“Sijajaribu kila aina ya nyoka mwenye sumu. Lakini, nimeshang’atwa na nyoka wote ambao sumu yao huua kwa haraka.”


Ana makovo tele mwilini kutokana na majaribio yake hayo, na ameshawahi kukaribia kifo mara kadhaa. Lakini bado anakubali kushambuliwa bila ya uwepo wa madaktari.


“Kama mara 12 hivi nilipata taabu kwenye kupona. Katika mwaka wangu wa kwanza ilinibidi nilazwe hospitali baada ya kushambuliwa na swila wawili. Ni lazima ukutane na shida kwenye kujifunza. Hakuna daktari ama Chuo Kikuu Chocote Duniani kinachoweza kukufunza haya.”


Si wote ambao wanampinga kwenye ulimwengu wa sayansi.


Mwenyewe anasema kuwa njia yake hiyo ya kupambana na sumu ya nyoka imedhihirika kuwa inafaa baada ya vipimo vya maabara.


Miaka miwili iliyopita video zake zilimgusa mtaalamu mmoja wa masuala ya kinga, Jacob Glanville, ambaye aliacha kazi kama mwanasanysi mkuu wa kampuni kubwa ya kutengeneza dawa ya Pfizer ili kuanzisha kampuni binafsi inakayojikita kwenye dawa za sumu ya nyoka.


“Alichokifanya Fredie ni cha kustaajabisha, lakini ni hatari sana na siwezi kumshauri yeyote amuige,” amesisitiza Glanville.


Lakini kampuni yake inatumia sampuli ya damu ya Friede kutengeneza dawa dhidi ya sumu hizo.A researcher experiments on a lab mouse at a laboratory in China


Dawa mpya mara nyingi hutumiwa kwa panya ili kupima ufanisi wake

“Walichukua vinasaba vyangu na kuzizalisha zaidi maabara. Hii ni sayansi ya hali ya juu,” amesema Friede.


Endapo majaribio yao yatazaa matunda na kutengeza kinga basi Friede tapata kiasi kikubwa cha fedha.


“Hauwezi kung’atwa na nyoka ili upate pesa. Lakini kama tutaweza kutengeneza kinga mpya itaingiza fedha nyingi sana. Tayari nina mwanasheria na nimeshaini mkataba,” anaeleza Friede.


Glanville anaamini kuna mafanikio makubwa mbele yao.


“Utafiti upo katika hatua ya mbali sasa – twakaribia kuanza kuijaribisha kwa panya.”


Wawili hao wanapingwa vikali na jamii ya wanasayansi kwa njia wanazotumia kuthibitisha nadharia yao, lakini wenyewe wanajitetea vilivyo.


Glanville anasema wamechukua tahadhari zote za kisayansi.


“Kuna lengo kuu nyuma ya majaribio yangu hatari. Najiweka kwenye mstari ili kutafuta kinga nafuu ya sumu ya nyoka duniani,” anajitetea


Ugonjwa uliopewa kisogo

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kila mwaka watu milioni 5.4 hung’atwa na nyoka. Idadi ya vifu huwa baina ya watu 81,000 na 138,000. Zaidi ya 400,000 hupata ulemavu wa kudumu.


 Lakini baada ya ukimya wa muda mrefu, mwaka 2017 WHO ikatangaza rasmi kuwa kung’atwa na nyoka ni ugonjwa uliopewa kisogo.


Kila mwaka, Septemba 19 huadhimishwa kama siku ya kukuza ufahamu juu ya mashambulizi ya nyoka.


Lengo ni kuchochea mjadala kwa jamii juu ya tatizo ambalo linawaathiri sana wakaazi wa vijijini barani Asia, Afrika na Amerika ya Kusini ambao mifumo yao ya huduma za afya ingali duni.


Katika nchi nyingi, hususani masikini, dawa zilizopo hazifanyi kazi ipasavyo, sababu ya kuhifadhiwa vibaya ama hutibu aina fulani tu ya nyoka na si wote.


Mwezi Mei mwaka huu Wellcome Trust ilitangaza kuzindua mfuko wa dola milioni 100 kwa ajili ya tafiti ya dawa madhubuti.


Taasisi nyengine kadhaa pia zipo katika mawindo ya kupata dawa mpya madhubuti na salama

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad