Argentina yazindua matumizi ya chanjo ya Covid 19 kutoka Urusi





Argentina leo hii imezindua kampeni ya matumizi ya chanjo ya Covid-19 iliyotengeneza Urusi ya Sputnik V. Na hivyo kulifanya taifa hilo kuwa la kwanza katika upande wa mabara ya Amerika kutumia chanjo hiyo. 
Waziri wa Afya, Gines Gonzalez Garcia amesema zoezi la chanjo limeanza kwa kupewa kipaumbele wafanyakazi wa sekta ya afya. 

Amesema hayo katika hospitali ya Posadas, ambako daktari Flavia Loiacono amekuwa mtu wa kwanza kuchanjwa chanjo hiyo nchini humo. 

Takribani dozi 300,000 zimewasili nchini humo katika siku ya mkesha Siku Kuu ya Krismas. Kiwango kingine cha dozi milioni 19.7 kinatarajkiwa kufika katika kipindi cha Januari na Februrari. 

Argentina ambayo ugonjwa wa Covid-19 umewauwa watu 43,000 imekuwa taifa la nne katika eneo la Amerika ya Kusini kuzindua kampeni za chanjo, baada ya Mexico, Costa Rica na Chile.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad