Polisi wawili na wafanyabiashara wakubwa wa madini wawili na mchimbaji mdogo wa madini mmoja, wamefunguliwa mashtaka kwa tuhuma za kutorosha madini katika tukio lililotokea Novemba 25 mwaka huu wilayani Chunya mkoani Mbeya.
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amewataja watuhumiwa hao ni Askari Polisi Koplo Hassan Njujilo mwenye namba E.8970 na Askari Polisi Daniel Mrema mwenye namba G.7757 wote wa Wilaya ya Chunya.
Watuhumiwa wengine ni wafanyabiashara ya madini akiwemo Sabra Ally na Malof Nassor na mchimbaji mdogo wa madini Hamdun Mtafuni wote wa kutoka Wilaya ya Chunya.
DPP amesema Novemba 25 mwaka huu, Askari hao wawili walikamata mzigo wa madini ya dhahabu iliyokuwa ikitoroshwa na waliomba rushwa ya Sh milioni 150 kutoka kwa wafanyabiashara hao, na kuachia mzigo huo.