Billion 1.5 Kumng’oa Luis Simba, Pyramid Yatua Bongo




IMEELEZWA kuwa matajiri wa timu ya Pyramid kutoka nchini Misri wapo tayari kuipa Simba Bilioni 1.5, kwa ajili ya kuvunja mkataba wa winga wa timu hiyo Luis Miquissone ili kumsajili kupitia dirisha dogo la usajili.

 

Luis tangu alipojiunga na Simba akitokea UD Songo ya Msumbiji amekuwa mchezaji muhimu zaidi kwa timu hiyo kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, mmoja kati ya kiongozi wa Simba ambaye jina lake hakutaka litajwe, alisema kuwa ni kweli kuna baadhi ya timu zimeonyesha nia ya kumuhitaji mchezaji huyo tena kwa kuvunja mkataba wakiwemo Pyramid na timu moja kutoka Ureno.“

 

Luis Miquissone ana mkataba mrefu sana na Simba ambao kuuvunja lazima ulipie kiasi kikubwa sana lakini hilo halijafanya timu ziache kumuhitaji mchezaji huyo kwani tayari kuna timu ya Pyramid ya Misri na moja kutoka Ureno ambazo zipo tayari kulipia si chini ya bilion 1.5 ili kumsajili.



“Ndiyo maana utaona baada ya mechi ya pili ya ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau Mwenyekiti wa Bodi, Mohammed Dewji alikutana na Luis kuzungumza naye ambapo mazungumzo yao yalihusiana na ofa hiyo kutoka Pyramid na hatma yake klabuni hapo,” alisema kiongozi huyo.

 

Championi Jumatatu, lilimtafuta Mkuu wa idara ya Uendeshaji wa Simba, Arnold Kashembe kuzungumzia juu ya dili hili lakini simu yake iliitwa bila kupokelewa.

 

Hata hivyo, taarifa tulizozipata kutoka chanzo chetu cha kuaminika ndani ya Simba kimelithibishia Championi Jumatatukuwa mkataba wa Luis una thamani ya Bilioni 1.3, Jambo ambalo limesababisha Pyramid kuongeza milioni 200 kumpata mchezaji huyo

Stori: MARCO MZUMBE, Dar es Salaam


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad