Mgombea urais wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, amesema Rais wa Yoweri Museveni anakabiliana na kizazi ambacho kitafanya kila iwezelo kupigania uhuru.
Alisema hayo katika hafla ya maombi iliyoandaliwa katika makao makuu ya chama chake kuwaomea watu waliouawa katika maandamano ya siku mbili yaliyokumba nchi, siku moja baada ya kuachiwa kutoka kizuizini.
Akimlenga moja kwa moja kiongozi wa nchi moja kwa moja Bobi Wine alisema Bwana Museveni anakabiliwa na kizazi ambacho kina njaa na hasira kwa wakati mmoja.
Mgombea huyo wa urais amesema mashambulio yaliyofanywa dhidi ya raia wiki hii yameweka wazi udhalimu wa serikali ya sasa iliyo madarani.
Akiwahutubia wafuasi na maafisa wa chama, alisisitaiza kwamba damu ya raia wasiokuwa na hatia iliyomwagika wiki hii haitaenda bure, na kuongeza kuwa haki itatekelezwa.
Jumamosi asubuhi, magari ya vikosi vya usalama yaliegeshwa katika maeneo tofauti mjini Kampala huku askari wakishika doria katika maeneo karibu na makao makuu ya chama cha upinzani cha People's Power.
Polisi imetangaza kuwa ni watu 28 waliofarika katika maandamano ya siku ya Jumatano na Alhamisi, japo vyombo vya habari nchini vinanukuu vyanzo vya hospitali kuu kwamba idadi ya waliofariki ni watu 37.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
PROMOTED CONTENTMgid
10 Advantages Of Dating Older Men
Herbeauty
These 9 Foot Shapes Reveal Unexpected Things About Personality
Herbeauty