Chama Mikononi Mwa GSM, Siku Ya Kutua Yaandaliwa




MEFAHAMIKA kuwa, Yanga imemalizana kwa siri na kiungo mchezeshaji wa Simba, Mzambia, Clatous Chama huku ikimfanyia kufuru kubwa nyota huyo.Mzambia huyo ambaye ni kipenzi cha Simba, kama kila kitu kitaenda sawa, basi atatua kuichezea Yanga kuanzia msimu ujao ikiwa ni baada ya mkataba wake wa miaka miwili ndani ya Simba kumalizika.

 

Kiungo huyo alikuwa kwenye mipango ya muda mrefu ya kusajiliwa na Yanga ikiwemo katika usajili mkubwa msimu huu, lakini mkataba wake ndiyo ulizuia mipango hiyo kukamilika.



Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Kampuni ya GSM ambao ndiyo wanaofanikisha usajili Yanga, wamefanya kufuru kubwa Chama ya kumjenga nyumba ya kisasa na kifahari nyumbani kwao Zambia.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, GSM imemjengea nyumba kiungo huyo katika sehemu ya masharti aliyowapa matajiri hao huku akiomba dau kubwa la usajili ambalo huenda likaweka rekodi.Aliongeza kuwa, pia kiungo huyo ameahidiwa gari la kutembelea la kifahari atakalolitumia katika matembezi yake ya binafsi sambamba na nyumba atakayoishi hapa nchini akiwa anaichezea Yanga.“

 

Hadi kufikia Januari 6, 2021, mkataba wa Chama na Simba unabaki miezi sita rasmi, hivyo anakuwa katika sehemu nzuri ya kufanya mazungumzo ya awali na klabu nyingine itakayomuhitaji.“Kwani kanuni za usajili za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), mchezaji anakuwa huru kufanya mazungumzo na klabu yoyote inayomuhitaji mkataba wake utakapobaki miezi sita.“



Hivyo, tarehe hiyo Yanga watakuwa katika nafasi nzuri ya wao kumpa mkataba wa awali, licha ya kuwepo taarifa za nyota huyo kusaini mkataba wa awali kwa siri ili Simba ambao wamiliki wa mchezaji huyo wasijue.“

 

Kwani tayari kiungo ameshajengewa mjengo mkubwa nyumbani kwao Zambia na mabosi hao wa Yanga katika kutimiza masharti ambayo Chama amewapa kama kweli wanaihitaji saini yake,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, hivi karibuni alitoa kauli ya kutisha kwa kutamka kuwa: “Tupo tayari kumsajili mchezaji yeyote kwa gharama yoyote ndani ya Afrika, kikubwa tu kocha amuhitaji.”

 

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, bilionea Mohammed Dewji, alitoa ahadi ya kumbakisha Chama Simba kwa kumuongezea mkataba mpya wa kuendelea kuichezea timu hiyo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad