LICHA ya kwamba alitangulia kwenye gemu lakini anachokifanya kwa sasa ni kama staa wa muziki kutoka Uganda, Joseph Mayanja ‘Chameleone’ anamuiga staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa kuja na kituo cha televisheni.
Chameleone amepanga kuanzisha televisheni yake ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 kwenye gemu la muziki. Mkongwe huyo kwenye gemu alikuwa na ndoto ya kumiliki chombo cha habari muda mrefu na sasa ndoto yake inakwenda kutimia ambapo kila kitu kipo tayari na kituo hicho cha luninga amekipa jina la The Leone TV.
Jina hilo limekuja baada ya kuwepo kwa studio ya kurekodia muziki inayokwenda kwa jina la Leone Record Label. Ni dhahiri kwamba sasa Chameleone anakwenda kuwa sawa na Diamond ambaye anamiliki Wasafi Media ambayo ina Wasafi TV na Radio.