Chanjo ya Oxford-AstraZeneca imeidhinishwa kwa matumizi nchini Uingereza, huku dozi ya kwanza ikianza kutolewa Jumatatu wakati ambapo visa vya virusi vya corona vinaendelea kuongezeka.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametaja maendeleo ya chanjo hiyo "ushindi mkubwa" kwa sayansi Uingereza, na kuongeza kuwa: "Sasa tutaanza kutoa chanjo hii kwa wengi haraka iwezekanavyo."
Pia utolewaji wa chanjo hiyo unatarajiwa kuwa wa juu zaidi wakati huu ambapo dunia inakabiliana na virusi vya corona hasa ukizingatia kuwa ni rahisi kuihifadhiwa na kuitengeneza kwa kiwango cha juu ikilinganishwa na chanjo nyingine.
Uingereza imeagiza dozi milioni 100 - inayoweza kutosheleza watu milioni 50.
Chanjo hii ilitengenezwa miezi ya kwanza ya 2020 ikafanyiwa majaribio ya kwanza April na tangu wakati huo maelfu ya watu wamekuwa wakipewa.
Uingereza pekee, zaidi ya watu 600,000 tayari wamepata chanjo hiyo na pia chanjo hii ya Oxford-AstraZeneca inatarajiwa kuleta mafanikio makubwa kwasababu bei yake ni ya chini na rahisi kutengenezwa na hivyo basi mataifa mengi maskini pia yanaitarajia.
Aidha, inaweza kuhifidhiwa katika jokofu la kawaida tu na kumaanisha kwamba itakuwa rahisi kufika katika vituo vya afya vya mashinani.