Kichwa cha farasi kilichoibwa miaka 160 iliyopita kimekuwa cha kwanza cha aina yake kurejeshwa nyumbani China.
Kichwa hicho ni moja ya vitu vya kale maarufu 12 vya michongo ya wanyama vilivyonakshiwa kwa shaba ambavyo viliibwa nchini China pale wanajeshi wa Uingereza na Ufaransa walipoivamia China wakati wa vita vya pili vya China.
Zaidi ya nusu ya bidhaa za kale tayari zimeshapatikana na kurejeshwa China lakini kwasasa zinaoneshwa katika maeneo mengine ya makumbusho.
Kichwa hicho cha farasi kilkabidhiwa China na aliyekuwa tajiri wa Macau Stanley Ho, aliyenunua bidhaa hiyo kwa dola milioni 8.9 za Marekani (£6.63m) kwenye mnada uliofanyika Hong Kong mwaka 2007 na baadaye akaiwasilisha kwa serikali ya China mwaka 2019.
Inasemekana, serikali ya China imetumiwa kipindi cha mwaka mzima kuboresha eneo itakapowekwa mchongo huo kulingana na chombo cha habari cha Xinhua.