MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga, amesema ni kosa kuwarejeshea fedha watu waliojiunga na kampuni ya Qnet kisha kudai wametapeliwa.
“Ni kosa kisheria kuwarejeshea fedha watu waliojiunga na Kampuni ya Qnet kisha kudai wametapeliwa kwakuwa kufanya hivyo ni kosa,” ameeleza.
Amefafanua hayo zikiwa zimepita siku mbili baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Geita kurejesha shilingi milioni 5.48 kwa mwalimu Rose Mgomba wa Shule ya Msingi Lukaranga aliyedai kutapeliwa na kampuni hiyo.
Mganga amesema urejeshwaji wa fedha hizo ni kosa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa biashara iliyokuwa inafanywa na kampuni hiyo ni ya upatu ambapo ipo katika kundi la biashara haramu.
So whats next.? TCRA..!! BOT..Usalama
ReplyDeleteau mchakachuaji alie kimbillia Kanada
anahusika na mtandao halamu.
Tunahitaji majibu na kompyuta baadhi ziko kituoni Arusha.