ABDALLAH Sultan, wengi wanamfahamu kama ‘Dullvan’ au ‘Da Zuu’. Ghafla tu huyu jamaa amekuwa ni miongoni mwa wasanii wa vichekesho wenye kuvutia Bongo.
Pia amepata mafanikio makubwa kupitia mitandao ya kijamii, bila kutumia jasho kupata umaarufu alionao hivi sasa tofauti na zamani ambapo iikuwa ni lazima uonekane kwenye runinga ndipo ujulikane.
Msanii huyu ambaye amekuwa kivutio kikubwa sana kwa watu wengi,kutokana na uigizaji wake,ambapo mwanzo alianza kwa kuwaigiaza mastaa wakubwa na wengi wao walimfahamu kupitia hivyo, huku wengine walikuwa hawapendezwi na jinsi wanavyoigwa na msanii huyo.
IJUMAA,lilipata nafasi ya kufanya nae mahojiano maalum(exclusive interview) kama ifuatavyo:
IJUMAA: Habari Dullvan?
Dullvan: Salama kabisa vipi hali?
IJUMAA: Mungu anatupigania,hongera kwa kazi nzuri, msomaji wangu angependa kufahamu ulifikiria nini mpaka ukaamua kuanza kuonyesha vichekesho vifupi kwenye simu?
Dullvan: Unajua mimi kipindi niko shule na hata chuoni,wezangu nikiongea nao au ukafanya kitu wanacheka sana,lakini mimi nikaona kawaida hivyo nikasema hebu nijaribu kujirekodi kweye simu nivitume kwenye Instagram,nione mapokeo yake lakini cha ajabu nikaona watu wanapenda sana.
IJUMAA: Kwanini ulipenda kuigiza kama mwanamke toka mwanzo.
Dullvan: Nilikaa na kuwaza,kwamba Mashabiki wengi wa mambo haya ya uigizaji ni wanawake na pili nilitaka kitu cha utofauti kabisa.
IJUMAA: Kuigiza kama mwanamke wakati mwingine kuna changamoto zake,kwa upande wako ni changamoto gani unakutana nazo hasa kwa upande wa familia?
DULLAVANI: Kwa wazazi wangu maana ni watu wa dini,mwanzo niliamua kufanya bila wao kujua lakini kutokana na Mitandao,walijua ambapo mama alinifuata na kuniuliza, baada ya kumwambia ni kazi tu,akaniambia kama ni kweli basi ananitakia baraka,lakini kwa wengine wanaweza kukufikiria tofauti kumbe ni kazi tu.
IJUMAA: Mara nyingi unawaigiza mastaa wakubwa,na kunakipindi pia ulimuigiza Diamond,hupati shida yeyote kwenye hilo,kukupigia simu kulalamika?
Dullvan: Kweli kabisa,kwa mfano Diamond,anajua sana sanaa, hata nilipomuigiza,akikutana na mimi anacheka sana,lakini niliwahi kumuigiza Wolper akanitukana,basi mtu wa namna hiyo anakuwa haijui sanaa yake vizuri.
IJUMAA: Sanaa hii ya vichekesho,imekuletea mafanikio gani?
Dullvan: Kwakweli mafanikio makubwa sana,nimeweza kufanya vitu vingi sana vya maendeleo kupitia kazi hii,kujulikana na watu mbalimbali lakini mama yangu kanishauri pia nirudi chuo.
IJUMAA: Ulikuwa unasoma chuo gani?
Dullvan: Chuo cha DSJ,hivyo nataka kuongeza ngazi ya juu kwenye chuo hicho.
IJUMAA: Kwahiyo unataka kuwa mwandishi wa habari?
Dullvan: Ndio,nataka kuwa na kampuni yangu.
IJUMAA: Kwa hivi sasa una familia?
Dullvan: Hapana,mimi naishi bado nyumbani kwetu na hata familia bado sijafikiria kuwa nayo kwasababu mimi bado mtoto.
IJUMAA: Kwenye uigizaji wako unavaa madira ya kike na mara nyingi uwa ni mapya,hivyo unakodisha unaigizia kisha unarudisha ua unanunua?
Dullvan: Ninanua na nina madira Kama 50,yaani ninayo mengi kuliko nguo zangu za kawaida.
IJUMAA: Simu yako iliyokuletea mafanikio uliyonayo ulinunua ya shilingi ngapi?
Dullvan: Nilinunua laki na nusu,lakini imeniletea mafanikio zaidi hata ya milioni 50.
IJUMAA: Haya nakushukuru sana Dullvan kwa ushirikiano wako.
Dullvan: Asante sana dada.
Makala: Imelda Mtema, Bongo