Asubuhi/alfajiri ni muda ambao watu wengi huutumia kufanya maandalizi ya siku itakavyokwenda. Wengi hutumia muda huo kujiandaa kwenda kwenye shughuli zao za kila siku, ili kuweza kujiingizia kipato.
Lakini Je! Ratiba za watu wote kwa kile wanachofanya asubuhi hufanana? Je! matajiri wakubwa duniani, na watu wengine wenye vipato vya kawaida hufanya vitu vya kufanana?
#TomCorley ambaye ni muandishi wa kitabu cha Rich Habits alifanya uchunguzi kwa mamilionea (matajiri) 233 kwa muda wa miaka mitano, na akabaini namna mamilionea hao wanavyowekeza katika muda wa asubuhi, jambo linalowasaidia kufanya vizuri kibiashara. Umeeleza mtandao wa Business Insider.
1: Hutafakari (meditation)
Hufanya tafakuri za mambo mbalimbali ikiwemo matatizo na vikwazo wanavyokumbana navyo katika shughuli zao, au kwenye kufikia ndoto na malengo yao au kwenye taaluma zao. Hii huwasaidia kupata ufumbuzi wa kukabilia na changamoto hizo na wakati mwingine huzigeuza kuwa fursa.
2: Husoma vitu vinavyoakisi ukweli (facts)
Hufanya hivi ili kuweza kukuza na kuboresha uelewa wao kuhusu masuala kadha wa kadha. Lakini pia husoma vitu vinavyowachochea na kuwatia moyo (uplifting, motivational na insperational) ili wawe sawa kiakili.
#Corley ameeleza kuwa hili ni muhimu sana kwani ili kuweza kufanikiwa ni lazima uwe na mawazo chanya, na kuyapata ni lazima ufanye vitu vitakavyo kufanya uwe juu. Vitu hivyo ni kutafakari na kusoma vitu sahihi.
Je! Wewe hufanya nini asubuhi kabla ya kwenda kwenye shughuli zako/ kuanza hizo shughuli?