MKURUGENZI wa Fettilicious Kiboko ya Vitambi, Fatina Deus almaarufu Fetty amemtaka staa mkubwa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu, aende ili amrejeshee mwili wake kama ule wa zamani.
Fetty amesema anatamani japo amrejeshee Wema ule mwili wake ili aondokane na maneno ya watu ya kuambiwa amekondeana.
Amesema kuwa, pamoja na kwamba, yeye yupo kwa ajili ya kuwahudumia watu wanaohitaji kupunguza uzito salama, lakini atafanya hivyo kwa Wema. Fetty anasema kuwa, mara nyingi, dawa wanazotumia watu wengi kutoka nje ya nchi za kupunguza mwili, zina madhara makubwa hivyo ni vyema kutumia dawa ambazo hazina madhara wala kemikali zozote.
“Kiukweli natamani sana Wema aje nimrejeshee mwili wake, kuna vitu nataka kumshauri, lakini pia naomba watu wote wenye kuhitaji kupunguza miili yao kistaarabu, bila madawa yenye kemikali zozote, wanione kwa maana ninatumia mimea asili kabisa yenye kutibu magonjwa mbalimbali na mtu anapungua bila kutumia nguvu yeyote aje Instagram anitafute kwa jina la fettilicious_kiboko_ ya_vitambi,” anasema Fetty ambaye ni maarufu kwa mastaa ambao hawapendi ubongenyanya.
GPL