Afisa Uchaguzi wa jimbo la Georgia nchini Marekani, Gabriel Sterling ameonya kuwa Rais Donald Trump atachukua jukumu la ghasia zozote zitakazojitokeza kutokana na madai ya udanganyifu katika uchaguzi ambayo hana uthibitisho
Katika taarifa yake, Sterling, kutoka Republican, amesema ni muda kwa Trump kuachana na hayo mambo.
“Kila kitu kimeenda mbali sana! Yani kila kitu! Inabidi kuachana na haya mambo!”
Jimbo la Georgia limefanya marudio ya kuhesabu kura kwa mara ya pili baada ya kampeni ya Trump kuomba kura zirudiwe kuhesabiwa.
Rais mteule wa Marekani, Joe Biden kutoka chama cha Democratic alitangazwa kuwa na ushindi mdogo katika jimbo hilo.
Msemaji wa kampeni za Trump, Tim Murtaugh amesema anajaribu kuhakiki kuwa kura zote zilihesabiwa na hakuna kura zilizoibiwa.
“Mtu yeyote asijihusishe katika vitisho na ghasia, na kama zimetokea tunalaani vikali vitendo hivyo,”
Akizungumza kwa ghadhabu katika mkutano na waandishi wa habari huko Atlanta jana Sterling, msimamizi wa mfumo wa upigaji kura aliwakemea wanachama wenzake wa Republicans, pamoja na rais.
Amesema, kwa miaka 20 ambayo amekuwa akisimamia mfumo wa upigaji kura katika uchaguzi wa taifa hilo, nadharia ya kutokubalika kwa ushindi, kumesababisha apate vitisho vya kuuawa na familia za wafanyakazi wamekuwa wakisumbuliwa, ameongeza.
Mhhhhh....Mbona Makubwa !!! Mpaka Malekani Sanaa Mtindo Umoja.
ReplyDeleteSi bola na yeye aende kule wanapo endaga
ubeli Giji