Kampuni ya Marekani ya Google, imeitaka Serikali ya Uganda kuwasilisha kesi Mahakamani kuhusiana na ombi lake la kutaka kufunga baadhi ya Youtube channel.
Serikali ya Uganda kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini humo UCC, iliandikia Google ikitaka kampuni hiyo kufunga Youtube channel ya Ghetto TV na nyingine 13 kwa madai kwamba zimekiuka maadili na kuvunja sheria za upeperushaji habari nchini humo.
GhettoTV na stesheni nyingine kadhaa, zina uhusiano na Chama cha National Unity Platform, cha mgombea wa urais, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine.
Kulingana na vyombo vya habari nchini Uganda, kiongozi wa mawasiliano wa kampuni ya Google barani Afrika, Dorothy Ooko, amesema kwamba kampuni hiyo haiwezi kufunga channel hizo kwa sababu tu kwamba Serikali imetaka ifanyike hivyo.
“Ni vigumu sana kuondoa tu stesheni kwa sababu serikali nataka stesheni hiyo iondolewe kwenye You tube. Tunafuata sheria kila mara, lakini ni lazima iwe amri kutoka mahakamani. Barua zinaonyesha tu yake UCC imewasilisha kwa ubalozi. Sio amri ya mahakama,” Oooko.