Guinea yaanza kutoa chanjo za corona kwa mawaziri wa serikali




Taifa la Afrika Magharibi la Guinea limeanza kutoa chanjo za corona, na kuifanya kuwa miongoni mwa nchi za kwanza kwenye bara hilo kuzindua mipango hiyo kabambe. 
Mawaziri wameoneshwa kwenye televisheni wakipewa dozi zao katika kasri la rais jana usiku. 

Waliripotiwa kupewa chanjo ya Sputnik V inayotengenezwa Urusi, chanjo ambayo imezusha wasiwasi lakini ambayo pia inatumika katika maeneo kama Belarus na Argentina. 

Spika wa Bunge Amadou Damaro amesema baada ya kupewa chanjo hiyo kuwa dhamira ya kudumu ya serikali ni kupambana na ugonjwa huo. 

Nchini Guinea, maambukizi 13,680 yamerekodiwa mpaka sasa kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika. 

Watu 80 wamefariki dunia nchini humo kutokana na virusi vya corona.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad