“Hakuna madhara usipooga” Daktari aliekaa miaka 5 bila kuoga

 



James Hamblin ni daktari wa Marekani ambaye amekaa bila kuoga tangu mwaka 2015 akifanya utafiti wa kuona kama kuna madhara ya mtu kutooga mara kwa mara.


Amegundua hakuna madhara, harufu hutokana na bakteria kula mafuta yanayotolewa na mwili hivyo mtu akiacha kuoga kwa muda mrefu mwili unaacha kutoa mafuta, hivyo anakuwa hatoi harufu.


Anasema, mwanadamu hutumia wastani wa miaka miwili kuoga, muda ambao anaweza kuutumia kukuza Uchumi. Hata hivyo anasisitiza kunawa mikono na sabuni.


Hamblin ana umri wa miaka 37, na ni mtaalamu aliyesomea katika Chuo Kikuu cha Yale, Kitengo cha Huduma ya Afya ya Umma na ni Daktari Bingwa wa Tiba ya Kuzuia Magonjwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad