Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUf), Prof. Ibrahim Lipumba amezindua rasmi kongamano lenye lengo la kutetea maslahi na haki za wananchi nakusema kuwa uchaguzi wa mwaka huu alitegemea kuchukua viti 15 kwa upande wa ubunge.
Akizungumza katika uzinduzi wa kongamano hilo la Kudai katiba mpya, Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba ambaye alikuwa mgeni rasmi amelishukuru jeshi la polisi nchini kwa kuwaacha kuendelea na kongamano lao huku akihimiza kuzingatiwa kwa demokrasia nchini .
"Mkoa wa Kilimanjaro wamekuwa wanatoa wabunge wa upinzani lakini mwaka huu majimbo yote yamechukuliwa na wote wameenda kuunga juhudi, kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020 mimi nilikuwa na uhakika tutapata walau viti 15 vya ubunge" amesema Prof. Lipumba
Aidha Prof.Lipumba amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kuanza kusikiliza hoja za watanzania kuhusiana na suala la katiba mpya.